Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, idadi ya wakazi wa Basra leo wamekusanyika karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mji huo, wakipinga kuunga mkono Serikali ya Iraq vikwazo vya anga vya Marekani dhidi ya Iran.
Waandamanaji walikusanyika kuzunguka ndege ya Iran ambayo ilikuwa imesimama na kushindwa kuendelea na safari kutokana na kusitishwa huduma za uwanja wa ndege, wakitoa kaulimbiu dhidi ya Serikali ya Ali al-Zaidi, waandamanaji walieleza kuwa; hatua ya Baghdad ni kuunga mkono sera ya Washington ya kuizingira na kuiwekea Iran shinikizo.
Waandamanaji walisisitiza: Haki ya watu na mazuwari kusafiri na kutembeleana haipaswi kugeuzwa kuwa chombo cha Marekani cha kuwawekea shinikizo watu wa eneo hili.
Kusitishwa huduma kwa ndege za Iran, mbali na kuzuia mawasiliano ya anga kati ya Iran na Iraq, pia kumeleta matatizo katika safari za wagonjwa, wanafunzi na, hususan, ziara za mazuwari wanaokwenda katika Ataba Takatifu kutoka nchi zote mbili.
Maoni yako